Editor

Editor

  • Submitted By: Gikambi
  • Date Submitted: 07/30/2010 7:15 AM
  • Category: Biographies
  • Words: 294
  • Page: 2
  • Views: 399

Zanga aliketi sebuleni akiwaza na kuwazua. Msimu wa mvua ulikuwa umewaletea balaa na baraka.
Wazazi wake walikuwa wamekwamia pande za Lokichoggio.
Walikuwa wameenda kumtembelea Mjomba aliyehudumu katika kambi ya wakimbizi.
Vyombo vya habari vilisema barabara na daraja ziliharibiwa na mafuriko.
Wakati huo, Zanga alikuwa akiishi na Shangazi na Mjomba.
“Wazazi wangu watarudi lini?”
Zanga alimuuliza.
“Sijui watarudi lini lakini nimeambiwa kuna mipango ya kuwasafirisha
kwa ndege ya kijeshi,” Shangazi alimjibu.
“Na wasiporudi…”
Zanga alianza kulia.
“Nyamaza mpwa wangu. Lazima tujifunze kuwa na matumaini. Nitafanya juu chini kupata habari zozote kesho.,” alisema.
Zanga alishindwa kula wala kulala.
Akaomba ruhusa ya kutoenda shuleni.
“Shangazi, siwezi kusikiza chochote hadi nijue hali ya wazazi wangu,” aliwambia Shangazi.
Shangazi hakuwa na lingine bali kukubali ombi hilo.
Akawajulisha walimu wa mpwa wake kilichokuwa kikiendelea.
Baada ya siku nne Shangazi alipokea simu kutoka kwa afisa mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu.
Ilisema wazazi wa Zanga walikuwa salama salmini. Wangewasili nyumbani Ijumaa.
Furaha ya Zanga ilikosa kifani. Siku hiyo alilala usingizi wa pono akiota ndoto nzuri. Aliamka mapema na kujitayarisha.
Aliwaeleza marafiki zake kwamba wazazi wake wangewasilI Ijumaa.
Alhamisi jioni, Mjomba alipokea simu nyingine kutoka kwa shirika lilo hilo la Msalaba Mwekundu.
“Kutokana na hali mbaya ya anga, usafiri wote, wa angani na barabarani
umesimamishwa hadi hali iimarike.
Hakuna haja ya kuhatarisha maisha ya watu. Subira kidogo ingezaa
matunda mema,” afisa yuyo alisema.
Mjomba alipomwambia Zanga ujumbe huo, mwana wa watu alihuzunika
mno.
“Lazima ujipe matumaini. Tayari tumeambiwa wazazi wako wako salama.
Haja gani wajaribu kusafiri na kukwamia njiani au wapate ajali? Tulia Zanga. Mvumilivu hula mbivu,”
Mjomba alimwambia.
Alfajiri iliyofuata, wazazi wa Zanga walibisha mlango wa nyumba ya Shangazi na Mjomba.
Wenyeji waliwakumbatia kwa...

Similar Essays